Tutawaheshimu Club Africain - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Nov 2022
Tutawaheshimu Club Africain - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema pamoja na kutopata muda wa kutosha kujiandaa na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain, wamedhamiria kushinda mchezo huo

Nabi amesema watacheza kwa tahadhari kubwa akitambua ubora wa Club africain yenye wachezaji wengi chipukizi na mahiri katika mashambulizi ya kushitukiza

Kocha huyo raia wa Tunisia, amesema wanafahamu umuhimu wa mchezo huo na jambo muhimu kwao ni kupata matokeo mazuri hapa nyumbani

"Tunajua umuhimu wa mchezo huu kwetu kwa mashabiki na kwa Watanzania wote kwa ujumla na matarajio yetu ni kuhakikisha tunautumia Uwanja wa nyumbani kupata matokeo mazuri"

"Club Africain wana timu nzuri na Wachezaji wenye uzoefu pamoja na wachezaji chipukizi. Ni wazuri kwenye mipira ya kufa na mashambulizi ya haraka, pamoja na kwamba tunahitaji matokeo mazuri nyumbani pia tutacheza kwa tahadhari tusiruhusu goli"

"Wachezaji wako tayari na wameahidi kupambana, tunaomba sapoti kwa Mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi, nguvu yao ni muhimu sana kwenye mchezo wetu wa kesho," alisema Nabi

Katika hatua nyingine Nabi ameeleza masikitiko yake kutokana na ratiba ya mechi mfululizo ambazo kikosi chake kimecheza kwenye ligi na kupelekea baadhi ya nyota wake muhimu kupata majeruhi

Nabi amebainisha kuwa uongozi wa Yanga uliomba mchezo dhidi ya Geita Gold uahirishwe hawakukubaliwa

"Muda ni mchache, tumetoka kwenye ratiba ngumu na mechi zilikuwa zinafatana. Tuliliomba Shirikisho letu kusogeza mbele mchezo wetu wa Ligi dhidi ya Geita Gold lakini hatukupata majibu tuliyoyatarajia. Ratiba hii imetuletea majeruhi kwa baadhi ya wachezaji"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’