Gueldich ampinga Zahera kuhusu Djuma

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Nov 2022
Gueldich ampinga Zahera kuhusu Djuma

Kocha wa viungo wa Yanga Helmy Gueldich amesema mlinzi wa kulia Djuma Shaban ni miongoni mwa wachezaji waliotumika sana katika kikosi cha Yanga na hata wakati yuko AS Vita

Hivi karibuni kocha wa zamani wa Yanga Mwinyi Zahera aliibua mjadala kuhusu Djuma akidai hayuko kwenye kiwango bora baada ya kuongezeka uzito

Prof Gueldich amesema Djuma hakuongezeka uzito bali amepungua kulingana na uzito aliokuwa nao msimu uliopita

"Huyo anayesema ameongezeka uzito ni nani? Djuma yuko katika uzito muafaka wa mwili wake (kilo 73-75) tena bora kushinda msimu uliopita"

"Wangesema hivyo msimu uliopita ningewaelewa lakini sio sasa. Inawezekana kuna sababu ambazo zimemfanya Djuma kutokuwa bora uwanjani, lakini mimi kama mtu ambaye nasimamia mazoezi yao hilo naona sio sahihi"

"Huyu ni mmoja kati ya wachezaji waliocheza mfululizo sana hapa kwa rekodi nilizonazo, kuna wakati mchezaji anaweza kupungua ubora nafikiri hii ni changamoto ambayo Djuma anaipitia kwa sasa, " Gueldich alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

Djuma hakujumuishwa kwenye kikosi kilichosafiri Tunisia akisumbuliwa na majeraha ya nyama za paja

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’