Leo saa 2 usiku kwa saa za Tanzania Yanga itakuwa uwanja wa Hammedi Agrebi Olympic huko Tunisia kumenyana na Club Africain katika mchezo wa kuwania tiketi ya kutinga makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Yanga inashuka uwanjani huko Tunisia ikiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Jumatano iliyopita
Hivyo katika mchezo wa hii leo Wananchi wanahitaji kushinda au kupata matokeo ya sare ya mabao
Kwa maana nyingine leo Yanga inahitaji kufunga bao/mabao huko Tunisia ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga makundi
Jana Yanga ilifanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja wa Hammedi Agrebi Olympic, dimba lenye viwango vya Kimataifa
Ari na morali ya wachezaji iko juu, wanafahamu usiku wa leo watakuwa na dakika 90 muhimu sana ambazo kama watazitumia vyema, wataingia katika vitabu vya kumbukumbu vya klabu ya Yanga na majina yao yatazungumzwa katika miaka mingi ijayo
Mechi itapigwa saa 12 jioni kwa saa za Tunisia ambapo huku Tanzania ni saa 2 usiku

