Baada ya kipigo cha Yanga katika uwanja wao wa nyumbani, mabosi wa Club Africain wote wameachia ngazi
Rais na wajumbe wa klabu ya Africain jana walitangaza kujizulu nafasi zao baada ya kutupwa nje na Wananchi katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Alikuwa ni Stephane Aziz Ki aliyesababisha balaa hilo kwenye dakika ya 79 akiukwamisha mpira kimiani baada ya kupokea pasi ya kichwa kutoka kwa Fiston Mayele
Youssef Elmi Rais wa Club Africain amewaambia waandishi wa habari na wanachama wa klabu hiyo kuwa wamefikia uamuzi wa kujiuzulu kwa kuwa wameumizwa na matokeo yaliyokwenda kinyume na malengo yao kama viongozi kwa dhamana waliyopewa
Hawa Club Africain suluhu ya Dar iliwaponza, wakadhani wanawamudu Wananchi au walifikiri Yanga ni kama Kipanga Fc?