Kikosi cha Yanga kitaondoka jijini Dar es salaam kesho Jumapili kuelekea mkoani Singida kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji mabao utapigwa Jumanne, Novemba 22 kwenye uwanja wa Liti
Dodoma Jiji inacheza mechi za nyumbani katika uwanja wa Liti baada ya uwanja wa Jamhuri kufungiwa
Meneja wa Yanga Walter Harrison amesema kikosi kinaendelea na maandalizi kuelekea mchezo huo
Aidha Walter amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri akiwemo mshambuliaji Fiston Mayele ambaye alipata majeraha katika mchezo uliopita dhidi ya Singida Big Stars, mechi ambayo alifunga hat-trik
Vipimo vya kitabibu vilibainisha kuwa Mayele hakupata majeraha makubwa na tayari amesharejea mazoezini kujiandaa na mchezo huo
ADVERTISE HERE