Leo Dodoma Jiji watakuwa wenyeji wa Yanga katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa uwanja wa Liti mkoani Singida
Walima alizeti hao wameahidiwa kitita cha Tsh Milioni 30 kama watavunja rekodi ya 'unbeaten' ya Yanga
Baada ya kuona imekuwa ngumu kuizuia Yanga, kwa sasa kila mechi ambayo Yanga atacheza itakuwa kama fainali kwani wapinzani wao watakuwa wakipigania ahadi wanazopewa nje ya uwanja!
Kwa Yanga utaratibu wa bonus upo katika kila mechi, ushindi kwa Yanga katika kila mchezo unaambatana na bonus kwa wachezaji
Hii 'unbeaten' ya Yanga inawakera wengi hivyo kadiri inavyoendelea kudumu ndivyo ushindani unavyoongezeka kutaka kuisimamisha!
ADVERTISE HERE