Jana katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji ambao ulipigwa uwanja wa Liti mkoani Singida, Yanga iliwakosa nyota saba
Mlinda lango Djigui Diarra, Yannick Bangala, Juma Shabani, Farid Mussa, Bernard Morrison, Heritier Makambo na Stephane Aziz Ki wote walikosekana kutokana na sababu mbalimbali
Katikati ya mchezo pia Yanga ikampoteza nahodha wake Bakari Nondo Mwamnyeto ambaye aliumia na nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahim Bacca
Changamoto hiyo haikuizuia Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kuendeleza rekodi yao ya kutopoteza mchezo kwenye ligi sasa wakicheza mechi 48 mfululizo
Kama hawatapoteza mchezo unaofuata dhidi ya Mbeya City, Wananchi wataifikia rekodi ya mechi 49 iliyowekwa na Arsenal kule Uingereza mwaka 2004
Ni hivi; mafanikio haya ambayo Yanga wanaendelea kupata, ni kwa sababu ya ubora wa kikosi na benchi la ufundi
Kwa sasa Yanga haitegemei mchezaji mmoja kwani wameendelea kupata matokeo mazuri wakiwa kwenye mazingira tofauti
Zipo timu hapa nchini akikosekana mchezaji mmoja tu, basi ni tatizo kubwa lakini sio Yanga
Wachezaji wa Yanga pia wako timamu sana katika 'fitness', wamecheza kila aina ya mechi ngumu nyepesi na bado wakafanya vizuri
Kuna kila dalili Wananchi wanaweza kwenda msimu wa pili mfululizo pasipo kupoteza mchezo