Tuko tayari kuikabili Mbeya City - Kaze

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Nov 2022
Tuko tayari kuikabili Mbeya City - Kaze

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema kikosi kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 12 jioni

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Kaze alisema Yanga itaingia kwenye mchezo ikiwa na dhamira ya kushinda ili kuhakikisha wanatimiza malengo waliyojiwekea ambayo ni kutetea ubingwa

Kaze amesema Yanga haichezi kwa ajili ya kulinda unbeaten kwani sio malengo yao, bali wanahitaji kupata matokeo mazuri uwanjani na kufanikisha malengo ya timu mwisho wa msimu

"Tumejiandaa vizuri kwa sababu tunajua Mbeya City mechi zao za karibuni wamefanya vizuri. Hatuna rekodi nzuri nao mchezo uliopita kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Ni timu ambayo imekuwa ikitupa changamoto ambayo tumejiandaa kuikabili"

"Ni kweli tuna takwimu nzuri ambayo ni heshima kwa Klabu. Lakini hatuchezi kwa sababu ya rekodi ya unbeaten, tunacheza kushinda ili tufikie malengo yetu. Kwenye mafanikio yetu hatuna malengo ya unbeaten, tuna malengo ya kutwaa mataji yaliyopo mbele yetu. Unbeaten ni matokeo sio mafanikio. Sisi tunataka mafanikio," alisema Kaze

Kaze amesema wachezaji Stephane Aziz Ki na Djigui Diarra wamerejea kikosini baada ya kumaliza kutumikia majukumu ya timu za Taifa

Mchezaji ambaye atakosekana kesho ni Feisal Salum 'Fei Toto' ambaye anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano

"Aziz Ki na Djigui Diarra wamerejea kutoka kwenye majukumu ya timu zao za Taifa. Vile vile Yannick Bangala amerejea baada ya kumaliza adhabu yake ya kadi tatu za njano"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’