Baada ya Yanga kupoteza mchezo dhidi ya Ihefu Fc, kuna waliotamani matokeo hayo yawavuruge Wananchi na pengine kuwaondoa 'kwenye reli'
Lakini haikuwa hivyo kwa kiasi kikubwa, mashabiki wa Yanga wamewapa heshima wachezaji wao na benchi la ufundi kwa kucheza mechi 49 mfululizo pasipo kupoteza kwenye ligi
Kilichotokea jana kwa Yanga ni matokeo ya mpira wa miguu, hakuna timu itacheza milele pasipo kupoteza mchezo
Yanga imeandika rekodi mpya kwa Tanzania na Afrika Mashariki na ya nne duniani baada ya kucheza mechi 57 katika mashindano yote ya ndani pasipo kupoteza
Rekodi hii sasa inakwenda kukaa kwenye vitabu vya kumbukumbu na pengine itachukua miaka mingi kuvunjwa
ADVERTISE HERE