Mikiki mikiki ya ligi kuu ya Wanawake 'Serengeti Lite' inaanza kutimua vumbi leo ambapo Yanga Princess wao watasubiri kesho Jumatano Disemba 07 kucheza mechi yao ya kwanza
Yanga Princess inafungua pazia la ligi hiyo kwa mchezo dhidi ya Fountain Gate Princess ambao utapigwa uwanja wa Uhuru
Baada ya usajili makini kufanyika, msimu huu Wananchi wana matumaini makubwa kwa timu yao ya Wanawake kutwaa ubingwa
Tangu ligi ya Wanawake ilipoanzishwa, Yanga Princess haijawahi kushinda ubingwa
Ni msimu ambao hakuna ambacho Yanga Princess wanapambania zaidi ya ubingwa

ADVERTISE HERE