Polisi Tanzania 'wametepeta' mbele ya Yanga katika uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Vijana wa Mwinyi Zahera walifanikiwa kuizuia Yanga kwenye dakika 45 za kwanza timu zikienda mapumziko zikiwa hazijafungana
Hata hivyo wakati wa mapumziko Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alifanya mabadiliko kwa kumtoa Tuisila Kisinda na nafasi yake kuchukuliwa na Bernard Morrison
Ni Morrison aliyetengeneza bao la kwanza kwenye dakika ya 47 akimtengenezea Jesus Moloko aliyeiandikia Yanga bao
Yanga iliendeleza utawala wake katika kipindi cha pili na kuongeza mabao mwengine mawili kupitia kwa Fiston Mayele na Clement Mzize
Pengine Wananchi wangeondoka na ushindi mnono zaidi kama wangetumia vyema nafasi nyingi walizotengeneza
Ni ushindi ambao unazidi kuikita Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 41


