Tunaweza kusema Mganda Khalid Aucho kwa sasa ndiye mbeba ramani ya mapambano ya kikosi cha Yanga kwenye kila mechi
Aucho amekuwa katika kiwango bora sana msimu huu na pengine ni mmoja wa wachezaji waliocheza dakika nyingi zaidi
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amekuwa na uhuru wa kufanya mabadiliko katika nafasi mbalimbali kwenye kikosi chake lakini ni mara chache sana anaweza kumuacha nje Aucho
Kama hutamuona Aucho ndimbani Yanga ikiwa inacheza basi ni majeruhi au sababu nyingine yoyote itakayomfanya asiwepo
Huyu ndiye Kamanda Mkuu pale katikati ya dimba, akiunganisha vyema safu ya kiungo na ushambuliaji

Msimu huu umekuwa mzuri sana kwake kwani hata changamoto ya majeraha yaliyokuwa yakimsumbua msimu uliopita hakuna
Hapa Tanzania wanamuita 'Dk Aucho' kutokana na umahiri wake pale dimba la kati lakini kule Uganda wanamuita 'The tank' kwa sababu ana 'mapafu ya mbwa', mchezaji anayezunguka kila mahali uwanjani