Jana katika mchezo dhidi ya Coastal Union uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0, winga Denis Nkane alishindwa kumaliza mchezo huo baada ya kupata majeraha
Nkane aliumia wakati Yanga ikiwa imemaliza nafasi zake tano za kufanya mabadiliko na hivyo kupelekea Wananchi kumaliza mchezo huo wakiwa na wachezaji 10 uwanjani
Imebainika kuwa Nkane aliumia mshipa mdogo unaosababisha nyonga kukunja. Nyota huyo anatarajiwa kufanyiwa vipimo zaidi ili kubaini ukubwa wa majeraha aliyopata na ni muda gani anaweza kuwa nje ya uwanja
Taarifa ya kitabibu iliyotolewa na daktari wa Yanga, Moses Etutu, imebainisha kuwa wanasubiri saa 48 mpaka 72 ili waweze kumfanyia Nkane kipimo kikubwa kujua madhara zaidi aliyoyapata na kutoa ripoti kamili kuwa Nkane atakuwa nje kwa muda gani