Mchezo wa watani wa jadi ligi kuu ya Wanawake kati ya Simba Queens dhidi ya Yanga Princess umemalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Alikuwa Wogu Succsess aliyefunga bao mahiri la kichwa dakika za majeruhi kwenye kipindi cha kwanza kabla ya Simba Queens kusawazisha kwenye kipindi cha pili kupitia Vivien Aquino
Yanga Princess walipoteza nafasi kadhaa za wazi hasa kwenye kipindi cha kwanza, pengine walistahili kufunga zaidi ya bao moja
Ulikuwa mchezo mzuri ambao umetoa taswira sasa Yanga Princess haina unyonge tena na iko tayari kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Wanawake msimu huu



ADVERTISE HERE