Kwa Aziz Ki watalaumu sana magolikipa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Dec 2022
Kwa Aziz Ki watalaumu sana magolikipa

Baada ya mlinda lango wa Azam Fc Ali Ahamada kutema shuti la Stephane Aziz Ki hapo jana Farid Mussa kuifungia Yanga bao la ushindi katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja Mkapa, kwa mara nyingine lawama amepewa Ahamada

Katika mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-2, Aziz Ki alikuwa mwiba kwa Azam Fc akifunga bao moja na kusababisha mabao mengine mawili likiwemo la mpira wa adhabu ambao Ahamada alitema kabla ya Farid kumalizia

Wale wanaomlaumu Ahamada walipaswa kufuatilia mechi zilizopita na wangebaini kumbe Ahamada sio kipa wa kwanza kukutana na mashuti ya moto ya Aziz Ki

Walinda lango wa timu za Mtibwa Sugar, Club Africain, Simba, Namungo Fc, Coastal Union wote wanafahamu ugumu wa kudaka mikwaju ya Aziz Ki

Kuna utani winga Denis Nkane ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii akidai kuwa hata huko kambini Avic Town wakiwa kwenye viwanja vya mazoezi shughuli za Aziz Ki huwa sio ndogo

Nkane akadai kesi zimekuwa nyingi kutoka sokoni huko Kimbiji kwani mashuti ya Aziz huwa yanakwenda kuangukia sokoni na kuharibu bidhaa za wafanyabiashara...!

Wanaolaumu magolikipa wanapaswa kuheshimu uwezo wa Aziz Ki na kukubali kuwa ni mahiri katika mipira hiyo iliyokufa

Unaweza kudhani hatumii nguvu anapopiga mashuti yake lakini usijidanganye! Ni fundi hasa wa kupiga mipira hiyo na miguu yake ina nguvu za ajabu!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’