Mshambuliaji Yacouba Songne amedokeza kuwa ni suala la muda tu ataanza kuitumikia Yanga katika awamu ya pili
Inafahamika Yanga inahitaji kupunguza mchezaji mmoja wa kigeni ili kumsajili Yacouba taarifa za ndani zikibainisha kuwa tayari walishaanza mazungumzo na mshambuliaji Heritier Makambo
Kama mwafaka utafikiwa Yacouba anaweza akawa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Mtibwa Sugar Disemba 31 uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro
Yacouba na Lazarus Kambole wamekuwa sehemu ya kikosi cha Yanga wakifanya mazoezi na wenzao ili kuimarika baaada ya kupona majeraha
Winga Tuisila Kisinda alisajiliwa kuchukua nafasi ya Kambole ambaye alipelekwa Uganda kwa mkataba wa muda mfupi
Kambole amerejea akiwa 'fit' nae anamuweka kwenye wakati mgumu Kisinda ambaye bado hajafikia matarajio ya Wananchi