Yanga imejipanga kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Kocha wa magolikipa Soud Slim amesema wamekiandaa kikosi kukabiliana na Mtibwa Sugar katika mazingira yoyote
Slim ambaye amewahi kuinoa klabu ya Mtibwa Sugar, amesema wanatarajiwa mchezo mzuri wenye ushindani kwani wanatambua ubora wa Mtibwa Sugar katika msimu huu
"Tunaamini mechi yetu dhidi Mtibwa Sugar itakuwa nzuri kwa kuwa timu tunayocheza nayo imekuwa bora msimu huu na sisi tumejipanga kufanya vizuri"
"Tumejiandaa vyema kuwakabili Mtibwa Sugar katika hali yoyote, iwe mvua, liwe jua tuko tayari," alisema Slim
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, mshambuliaji Yusufu Athumani amewataka Mashabiki na Wanachama wa Yanga waendelee kuiombea timu yao wakiwa na dhamira kushinda mchezo huo pamoja na mechi zilizobaki
"Tunawaomba mashabiki wa Yanga waendelee kutuamini na kutuombea kwani tupo tayari kupambana ili tuweze kupata ushindi katika mechi zote zilizobakia," alisema