Hii Yanga ni kubwa sana, iheshimiwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jan 2023
Hii Yanga ni kubwa sana, iheshimiwe

Kama kuna watu wanamfundisha Feisal Salum kupimana ubavu na Yanga basi wanakosea sana

Kwani kwa hali ya kawaida siamini kama Feisal aliyeitumikia Yanga kwa jasho na damu anaweza kufanya hayo ayafanyayo mitandaoni

Njia pekee ya Yanga kumruhusu Feisal aondoke ni kufuata taratibu, na sio vinginevyo

Bahati mbaya bado ana mkataba wa zaidi ya mwaka mmoja na nusu hivyo, hizi sinema anazofanya mitandao zinaweza kuja kumgharimu baadae

Badala ya kutumia mitandao ya kijamii kuwapiga vijembe viongozi wake na 'kuwarusha roho' mashabiki wa Yanga, nafikiri alipaswa kutumia muda huo kuwaambia hao wanaotaka kumsajili wafuate taratibu

Namkumbusha tu, Yanga hii ina historia kubwa katika nchi hii, ni Taasisi kubwa ya michezo pengine kuliko zote hapa Tanzania

Haiwezi kuyumbishwa na mchezaji mmoja, asome historia ya Yanga, ataelewa

Mwanzoni wapo mashabiki wengi wa Yanga waliunga mkono jitihada zake za kudai maslahi zaidi, wanafahamu kwa ubora alioonyesha, pengine alistahili zaidi ya kile alichopata

Lakini uungwaji mkono huo ataupoteza kwani sasa ni kama anaikosea heshima Yanga

Pengine anatengeneza mazingira 'kuwakera' Wananchi ili waamue kuvunja mkataba wake na kumruhusu anondoke bure

Bahati mbaya imeshafahamika wapi anataka kuelekea, yawezekana kabisa kama hatafuata taratibu, anaweza akakaa muda mrefu sana pasipo kucheza mpira

Kama Yanga itamuhitaji kambini atapaswa kwenda na kama hatafanya hivyo basi asubiri rungu la kufungiwa na FIFA

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’