Siku 624 za Nabi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jan 2023
Siku 624 za Nabi Yanga

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi ametimiza jumla ya siku 624 tangu alipoanza kuinoa timu hiyo akiwa ameiongoza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara moja, Ngao ya Jamii mara mbili, Kombe la Shirikisho la Azam mara moja lakini pia kuiongoza kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.

Kana kwamba haitoshi, takwimu zinaonyesha katika mashindano ya ndani ambayo Nabi ameiongoza Yanga, timu hiyo imepoteza mechi tatu tu ambazo mbili ni za Ligi Kuu na moja ni ya Kombe la Shirikisho la Azam na zilizobakia ni ama imeibuka na ushindi au kutoka sare.

Achana na dondoo hizo za hapo juu, Nabi ameibuka na jambo lingine la kibabe ambalo hakuna kocha yeyote wa timu ya Ligi Kuu ya NBC ambaye ameweza kulifanya katika kipindi cha siku 624 ambazo Mtunisia huyo ameiongoza Yanga.

Ubabe huo wa Nabi ni ule wa kuwa kocha pekee ambaye hajaonja ladha ya kutimuliwa tangu alipotua hapa nchini kwa mara ya kwanza.

Tangu Nabi alipoanza kuinoa timu hiyo, Yanga ndio timu pekee ambayo hadi sasa haijabadilisha kocha mkuu huku nyingine 15 zikiwa zimeshabadilisha makocha kuanzia wawili na kuendelea.

Nabi ameshuhudia makocha wenzake wa timu nyingine wakibadilishwa na kuletwa wengine ambao baadhi humuacha huku yeye akiendelea kutamba katika viunga vya Jangwani.

Katika kipindi cha siku 624 ambazo Nabi amedumu Yanga, Simba imenolewa na makocha watano tofauti ambao ni Didier Gomez, Hitimana Thiery, Pablo Franco, Juma Mgunda na sasa Robertinho Olivieira wakati Azam imenolewa na makocha wanne tofauti ambao ni George Lwandamina, Abdihamid Moalin, Denis Lavagne na Dani Cadena.

Akizungumzia kudumu kwake ndani ya Yanga, kocha Nabi alisema ni kutokana na imani kubwa ambayo klabu imeweka kwake

"Nawashukuru viongozi, benchi la ufundi, mashabiki na wachezaji kwa ushirikiano mkubwa ambao wamekuwa wakinipatia. Haya yasingetokea kama tusingekuwa tunashirikiana. Naamini tutafanikiwa zaidi kama tukiendelea kuwa pamoja," alisema Nabi.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
9h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
13h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
14h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
14h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’