Kikosi cha Yanga kitaingia kambini kesho Alhamisi Januari 12 2023 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc
Mchezo huo utapigwa Jumatatu, Januari 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 12:30 jioni. Huo utakuwa mchezo wa kwanza wa ligi kuu kwa mwaka 2023
Hii ni mechi ya kisasi kwa Wananchi, hawa Ihefu Fc ndio walitibua rekodi ya 'unbeaten' wakiizuia Yanga kufikisha mechi 50 pasipo kupoteza kwenye ligi
Wakati ule Ihefu Fc waliifunga Yanga ilikuwa imejaa 'uchovu' baada ya kucheza mechi mfululizo
Wakati huu wanakutana na Yanga ambayo iko timamu kwa asilimia 100, wachezaji wamepata muda wa kutosha wa kupumzika na wako tayari kwa mapambano
Wachezaji wa Yanga wanafahamu umuhimu wa mchezo huo katika kutimiza malengo yao ya kutetea ubingwa
Hesabu zinaonyesha Yanga wanahitaji kushinda mechi tisa ukiwemo mchezo dhidi ya watani zao Simba ili kurejesha ubingwa Jangwani kwa msimu wa pili mfululizo
Itakuwa ni mechi ya kisasi..!