Baada ya utambulisho wake kwa Wananchi hapo jana, mshambuliaji Kennedy Musonda anatarajiwa kutua leo na moja kwa moja kuelekea kambini Avic Town kuungana na wenzake
Yanga iko kambini Avic Town kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc ambao utapigwa Jumatatu, Januari 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Ikimpendeza kocha Nasreddine Nabi, Musonda anaweza kuwa sehemu ya mchezo huo kwani yuko 'fit'
Musonda ametoka 'kukimbiza' ligi kuu ya Zambia ambako alikuwa kinara wa kuzifumania nyavu akifunga mabao 11 katika mechi 17 akiwa na klabu ya Power Dynamos
Usajili wake unatajwa kuwa na thamani kubwa kwani Yanga ililazimika kununua sehemu ya mkataba wake uliobaki na Power Dynamos
Aidha nyota huyo alikuwa mbioni kujiunga na TP Mazembe kabla ya Rais wa Yanga Injinia Hersi Said kwa ushirikiano na Mtendaji Mkuu Andre Mtine kumuwahi uwanja wa Ndege wa Kitwe, Zambia na kumshawishi kutua kwa Wananchi
Ukisikia 'UMAFIA' kwenye usajili ndio huu...!