Beki wa Kimataifa wa Mali, Mamadou Doumbia ndiye aliyafunga usajili wa Yanga kwenye dirisha dogo lililofungwa Januari 15 2023
Ujio wa Doumbia unamaanisha kuwa beki huyo amechukua nafasi ya kiungo Gael Bigirimana ambaye bado uongozi wa Yanga haujatoa taarifa rasmi juu ya hatma yake
Aidha zipo taarifa kuwa Bigirimana ataendelea kubaki kwenye kikosi cha Yanga lakini atatumika kwenye michuano ya kombe la Shirikisho (CAF CC)
Mshambuliaji Lazarus Kambole amejiunga na klabu yake ya zamani Zesco United kwa mkopo wa miezi sita
Wachezaji 12 ambao wamesajiliwa kuitumikia Yanga kwenye ligi ni Djigui Diarra, Djuma Shaban, Joyce Lomalisa, Mamadou Doumbia, Yannick Bangala na Khalid Aucho
Wengine ni Jesus Moloko, Tuisila Kisinda, Fiston Mayele, Kennedy Musonda, Stephane Aziz Ki na Bernard Morrison