Mshambuliaji kinda wa Yanga Clement Mzize amesema wachezaji wote wako tayari kwakabili Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa hapo kesho
Mzize amesema yeyote atakayepewa nafasi na benchi la ufundi katika mchezo huo, anaamini atatimiza wajibu wake ili kuhakikisha wanapata ushindi
Akizungumzia nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza baada ya Yanga kumsajili mshambuliaji Kennedy Musonda, nyota huyo aliyepandishwa kutoka timu ya Yanga U20, amesema kila mchezaji ana umuhimu wake kwenye timu, benchi la ufundi linafahamu kila mchezaji atumike wakati gani
Mzize anaamini bado anao muda wa kuendelea kujifunza kutoka kwa Walimu na wachezaji wenzake, pia akiendelea kujituma ili afikie malengo yake
"Kila mchezaji ana umuhimu kwenye timu na mwalimu anaweza kunipanga mimi, Musonda au Mayele lakini kikubwa ni mwalimu anahitaji kitu gani kuelekea mechi husika"
"Najifunza vitu vingi, Musonda ndio kwanza amekuja hivi karibuni sijapata muda wa kujifunza kitu kutoka kwake lakini nimejifunza vitu vingi sana kutoka kwa Mayele"
"Najiona mbali sana kwa baadae haswa kama nitamsikiliza mwalimu anachoniambia na wachezaji wenzangu wanachonifundisha"