Yanga inavyowashangaza wengi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
27 Feb 2018
Yanga inavyowashangaza wengi
Nyota wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, wameifananisha Yanga na mwanariadha wa mbio ndefu anayeanza kushindana akikimbia taratibu, lakini mwisho wa siku anaibuka shujaa kwa wale ambao walitangulia mbele.

Abeid Mziba ‘Tekero’ aliyewahi kuichezea Yanga na Taifa Stars, alisema watetezi hao wa Ligi Kuu Bara waliuanza msimu huu vibaya kwa kujikongoja, ila kwa sasa wamekuwa watamu kiasi cha kusisimua mashabiki wa soka.

“Haikuaminiwa mwanzoni, lakini kwa siku za karibuni imezidi kushangaza wengi, mfano mzuri katika michuano ya kimataifa wengi walijua Yanga inaenda kupigwa ugenini kutokana na kupata ushindi kiduchu nyumbani, lakini ikawa tofauti,” alisema.

“Hata katika Kombe la FA, dhidi ya Majimaji Yanga ilitumia uzoefu wake kupenya robo fainali, hili ni jambo linalosisimua wengi.”

Naye winga wa zamani wa Simba, Ulimboka Mwakingwe, alisema kwa namna Yanga ilivyokuwa inaonekana imechoka, iliwafanya Simba kuona kazi yao ni nyepesi, lakini mambo yapo tofauti.

Naye Kocha Msaidizi wa Stand United, Athuman Bilal ‘Bilo’ amesema inachofanya Yanga ni kama unavyosema usemi wa ‘Simba mwenda pole ndiye mla nyama’.

“Kitu muhimu Yanga ikiimarishe kikosi chake, wasije wakaona wanasifiwa na kuamini wapo vizuri sana, ila jinsi wanavyopata matokeo hata kwenye uchovu ni funzo kwa timu nyingine juu ya kuwa makini na timu hiyo kwa sasa,” alisema Bilo.

“Ina kikosi kinachopambana kwa ajili ya klabu, hilo ni jambo zuri.”

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
30m ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
48m ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
54m ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE →