FT : Yanga 2-0 Namungo, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Feb 2023
FT : Yanga 2-0 Namungo, NBC PL

Yanga imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo Fc

Dickson Job ndiye aliyeitanguliza Yanga kwa bao la kichwa kwenye dakika ya 43 akimaliza mpira wa kona kutoka kwa Djuma Shabani

Job anaungana na Kibwana Shomari, Djuma Shabani, Yannick Bangala na Bakari Nondo Mwamnyeto ambao ni walinzi waliofunga mabao msimu huu

Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0. Kipindi cha pili Namungo walirejea wakiwa na kasi zaidi lakini kwenye dakika ya 51 Aziz Ki akafunga bao lake la tano msimu huu akitumia vyema makosa ya mlinda lango Deo Munish 'Dida'

Haikuwa bahati kwa Fiston Mayele kuongeza mabao yake kwani pamoja na jitihada zote hakufanikiwa kuweka mpira kambani

Kennedy Musonda nae alipata nafasi kadhaa lakini uimara wa Dida ulimfanya asifungue akaunti ya mabao kwenye ligi

Alama tatu muhimu zimebaki Jangwani, Wananchi wanaendelea kukaa kileleni kwa tofauti ya alama sita baad aya kufikisha alama 59

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
9h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
18h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’