Miili ilikuwa imechoka leo, muhimu ushindi tu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Mar 2018
Miili ilikuwa imechoka leo, muhimu ushindi tu
Kwa mara nyingine Yanga imeibuka na ushindi muhimu katika mchezo ambao wengi walikuwa hawaipi nafasi kubwa ya kushinda.

Yanga imeshuka uwanja wa Nangwanda sijaona mkoani Mtwara kuivaa Ndanda FC ikiwa ni siku tatu tu tangu itinge robo fainali ya michuano ya kombe la FA baada ya kuichapa Majimaji mabao 2-1 mkoani Ruvuma.

Yanga iliingia kwenye mchezo huo kwa tahadhari kubwa ikitumia zaidi mipira mirefu na mashambulizi ya kushitukiza.

Haukuwa mchezo mwepesi kwa wachezaji wa Yanga ambao ni dhahiri miili yao ingali na uchovu baada ya kusafiri umbali mrefu pamoja na kucheza michezo mfululizo.

Kwa mara nyingine mbinu za Mzambia George Lwandamina anayenyemelewa na timu yake ya zamani ZESCO, zimefanikiwa.

Lwandamina amekuwa akibadilisha mbinu zake kufuatana na aina ya mchezo na aina ya kiwanja kinachotumika.

Yeye amefanikiwa kuvunja rekodi ya kuondoka na ushindi Mtwara kwa mara ya kwanza jambo lililomshinda mtangulizi wake Hans van Pluijm.

Yanga ingeweza kufunga mabao hadi manne katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo hivyo haukuwa ushindi wa kubahatisha.

Ushindi dhidi ya Ndanda Fc una maana kubwa kwa wachezaji wa Yanga ambao sasa wanaamini wanaweza kushinda mahali popote.

Pia Yanga inakwenda kujiandaa na mchezo dhidi ya Township Rollers huku morali ya wachezaji ikiwa juu baada ya ushindi huu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’