Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amewasili Tunisia kuongoza mapambano kuelekea mchezo wa kwanza hatua ya makundi kombe la Shirikisho dhidi ya US Monastir
Mchezo huo utapigwa Jumapili Februari 12 katika jiji la Tunis
Wakati Yanga ikielekea Tunisia, Hersi alisafiri kwenda Dubai ikiwa sehemu ya majukumu yake kama kiongozi mkuu wa Yanga
Juzi aliitembelea timu ya Royal FC inayoshiriki Ligi daraja la tatu huko Falme za Kiarabu na kusaini makubaliano ya ushirikiano na Yanga
Katika uongozi wake Hersi amedhihrisha kuwa namba moja wa Yanga kwani yupo kila sehemu ambayo Yanga ipo
ADVERTISE HERE