Kesho Jumapili Yanga itakuwa uwanjani huko Tunisia kuwakabili US Monastir katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi michuano ya kombe la Shirikisho barari Afrika
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema wameongeza bonus kwa wachezaji ili kuhakikisha wanafanya vyema katika mchezo huo wanaoanzia ugenini
Hersi amesema matokeo ya ushindi yatakuwa na bonus yake lakini pia hata kama watapata droo wachezaji watapata bonus
"Awali shauku ya wapenzi, wanachama na mashabiki wa Yanga ilikuwa kuona timu yao inatinga hatua ya makundi, hilo tumelifanikisha, sasa kila mmoja anataka kuona tunafanya nini kwenye makundi"
"Malengo yetu ya awali ni kuona tunaweza kutinga robo fainali. Kwa umuhimu wa mchezo dhidi ya US Monastir, tumewaongezea wachezaji motisha ili kuhakikisha tunafanya vizuri"
"Huu ni mchezo ambao unaweza kutupa mwanga kuelekea malengo yetu. Kutakuwa na bonus ya ushindi lakini pia hata kama mchezo utamalizika kwa sare, kutakuwa na bonus pia. Katika michuano hii pointi moja ugenini nayo ina umuhimu mkubwa," alisema Hersi