Mashabiki wa Yanga leo walipata nafasi ya kuwasiliana na viongozi na wachezaji wao moja kwa moja kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa Jumapili, Februari 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Tukio hilo lilifanyika Zakiem Mbagala, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam
Wachezaji walitoa ahadi kwa mashabiki wao kuwa watahakikisha wanashinda mchezo wa Jumapili huku wakiwataka mashabiki wajitokeze kwa wingi dimba la Mkapa kuwashangilia
Mshambuliaji Fiston Mayele akawahakikishia Wananchi watarajie mambo makubwa kutoka kwake kwani amejipanga kufanya zaidi ya yale ambayo amewahi kuyafanya hata Tanzania
"Njooni kwa wingi uwanjani, nawaahidi Fiston Mayele mtakayemuona sio yule mliomuona mechi ya Zalan, Al Hilal na hata mechi ya Ngao ya Jamii. Tumejipanga kuwapa furaha mashabiki wetu hivyo mje kwa wingi," alisema Mayele


