Yanga kuwakabili TP Mazembe kivingine

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Feb 2023
Yanga kuwakabili TP Mazembe kivingine

Ni wazi Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi na benchi la ufundi wamefanyia kazi changamoto zilizojitokeza kwenye mchezo dhidi ya US Monastir ambao Wananchi walipoteza kwa kufungwa mabao 2-0

Katika mchezo huo, Yanga ilitawala kwa muda mwingi lakini waliadhibiwa kupitia mipira ya kutenga ambayo Monastir waliitumia kufunga mabao yao

Baada ya kutua kutoka Tunisia, Nabi alieleza masikitiko yake kwa vijana wake kuruhusu mabao hayo aliyoyaita mepesi

Nabi akaahidi watafanya kazi ya maboresho kwenye viwanja vya mazoezi ili kuhakikisha hawarudii makosa hayo katika mchezo unaofuata dhidi ya TP Mazembe na mechi zitakazofuata

TP Mazembe nao ni wazuri katika mipira ya kutenga hivyo ni lazima safu ya ulinzi ya Yanga kujiandaa kukabiliana nao

Kuhusu changamoto ya kutengeneza na kutumia nafasi iliyoonekana katika mchezo uliopita, kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze alisema mashabiki wa Yanga watarajie mabadiliko katika mchezo dhidi ya TP Mazembe

"Hii ni mechi muhimu sana kwetu. Hatukufarahishwa na matokeo ya mchezo uliopita, hii ni nafasi kwetu kutumia vyema uwanja wa nyumbani kupata ushindi. Wachezaji wametumika vyema mazoezini kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo uliopita"

"Ari na morali ya timu iko juu sana, nafikiri kila mmoja yuko tayari kwa mchezo huu muhimu kwetu," alisema Kaze

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
16h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’