Makamu wa Rais wa klabu ya Yanga Arafati Haji amewataka mashabiki wa timu hiyo kuhakikisha wanaelekea uwanja wa Benjamin Mkapa kuipa sapoti timu yao katika mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe
Mchezo huo utapigwa kuanzia saa 1 usiku Wananchi wakizihitaji alama zote tatu katika mchezo wa kwanza nyumbani
Arafat amesema Yanga leo ina majukumu mawili, moja ni kusaka ushindi na pili ni kurejesha na kuilinda heshima ya Taifa
"Hakuna sababu ya Mwananchi yeyote kubaki nyumbani leo. Kila Mwananchi ana wajibu wa kuhakikisha anafika uwanjani kuwaunga mkono wapambanaji wetu," alisema Arafat
Baada ya watani zao Simba kuchapwa mabao 3-0 na Raja Casablanca jana katika mchezo wa ligi ya mabingwa, Yanga leo ina wajibu wa kuhakikisha wanairejesha heshima ya nchi na kuitendea haki ahadi ya Mama, Rais wa nchi Dk Samia Suluhu Hassan