Mandawa aanika siri za Township Rollers

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
1 Mar 2018
Mandawa aanika siri za Township Rollers
Wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika, Yanga wamemegewa siri kuhusu namna ya kupata matokeo ya ushindi mbele ya Township Rollers ya Botswana,Machi 6.

Mshambuliaji Mtanzania Rashid Mandawa anayeichezea BDF XI ya Bostwana amewataka Yanga kuuchukulia mchezo huo wa raundi ya kwanza kwa uzito wa aina yake.

Mandawa amewapa maumivu wapinzani hao wa Yanga mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kuwafunga mabao matatu (hat trick) kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini humo.

“Kama ubora wa kikosi chao ni mkubwa, hakuna wa kuwazuia. Wanaitawala Botswana, nimecheza nao michezo miwili msimu huu kwenye ligi na katika michezo yote miwili namshukuru Mungu kwa sababu nimefunga awamu zote.

“Mchezo wa kwanza walitufunga kwao kwa mabao 3-2, lakini kwenye matokeo hayo nilifunga bao moja, tukiwa nyumbani nimeandika histori kwa kufunga mabao matatu.

“Udhaifu wao mkubwa ni namna ya kumzuia mshambuliaji mwenye matumizi mazuri ya nguvu na akili, kuna mabeki wao wa kutumainiwa ambao huwa wanacheza mara kwa mara ambao ni Simisani Mathumo na Mosha Gaolaolwe.

Aliendelea; “Hao jamaa wako vizuri lakini kama Yanga itamtumia mshambuliaji wa namna hiyo basi wanaweza kupata mabao, kingine ni lazima wahakikishe wanatengeneza presha za mashambulizi mfululizo ili kuwachanganya walinzi hao.”

Hata hivyo Mandawa ameuzungumzia pia ubora wa mabingwa hao wa Botswana kwa kusema ni uwepo wa washambuliaji wake na viungo hatari ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa ushirikiano.

“Township nawajua vizuri kwa sababu kwanza ni majirani zetu pili nimefanya majaribio kwenye hiyo timu kabla ya kujiunga na BDF XI, kuna wachezaji wanne ambao ni viungo wa pembeni na wengine ni viungo washambuliaji ukimuondoa, Maano Ditshupo ambaye ni kiungo mkabaji.

“Kuna jamaa anaitwa, Lemponye Tshireletso, Motsholetsi Sikele,Edwin Moalosi na Segolame Boy wote hao ni wachezaji wa kutizamwa na Yanga,haitakiwi waletewe mzaha hata kidogo.

“Kama watadhibitiwa hao inamaana hata mshambuliaji wao, Joel Mogorosi hatokuwa na madhara,Mgorosi sio mshambuliaji halisi lakini wanapenda kumtumia sana kwa sababu anauwezo wa kufunga,” alisema Mandawa.

Hesabu zao

Township Rollers imeonekana kuwa na hesabu kali dhidi ya Yanga kwa kocha wao, Nikola Kavazović kuwapumzisha wachezaji wake muhimu kwenye mchezo uliopita wa BWPL ambao walipoteza mbele ya BDF XI.

Kavazović aliwapumzisha wachezaji wake wote wa kikosi cha kwanza ambacho kilifanya kazi kubwa ya kuwaondoa, Al Merreikh ya Sudan kwa jumla ya mabao 4-2.

Na badala yake aliwaanzisha,Wagarre Dikago,Thato Bolweleng, Percy More, Kaone Vanderwesthuizen, Tshepo Matete, Gape Mohutsiwa, Ivan Ntege, Boy Lechana, Ntesang Simanyana, Galabgwe Moyana na Bogosi Mfila.

Huku wachezaji wake wachache wa kikosi cha kwanza wakiwa kwenye orodha ya wachezaji wa akiba,hata hivyo kocha wa kikosi hicho aliweka wazi kabla ya mchezo huo kutokana na ugumu wa michezo aliyokuwa nayo mbele.

Kabla ya kucheza na Yanga, Township Rollers itakuwa na kibarua kigumu,Jumapili cha kujaribu kutwaa taji lao la kwanza msimu huu kwa kucheza dhidi ya Orapa United kwenye kombe la Mascom Top 8.

Mbinu zao

Wakati wakiwa kwenye maandalizi yao ya mwisho ya kucheza mchezo wa ugenini nchini Sudan dhidi ya Al Merreikh,kocha wa Rollers, Kavazović alizungumza na mtandao wao rasmi na kusema ni aina gani ya soka ambalo walipanga kucheza.

“Tunaenda Sudan na mbinu ambazo zipo wazi,tutashambulia mpaka muda tutakao pata bao,baada ya hapo ndiyo tunaweza kuanza kuzuia,”aliuambia mtandao wao.

Huenda Kavazović akaja na mbinu hiyo hata kwenye mchezo dhidi ya Yanga.Benchi la ufundi la Yanga linatakiwa kuwa makini kwa kutambua huo ujanja.

Kutokana na Rollers kuanza vizuri ule mchezo wa raundi ya awali kwa kuwafunga Al Merreikh mabao 3-0 basi katika mchezo wa marudiano, Sudan walifanikiwa kimbinu kwa kupata bao licha ya kufungwa 2-1.

Vigogo wao wametua

Viongozi wa Rollers wametua nchini kwa ajili ya kutizama mazingira ya uwanja wa Taifa ambao utatumika kwa ajili ya mchezo huo wa kimataifa pamoja na kutengeneza mazingira ya pakufikia na mengineyo.

Waliotua nchini ni meneja wa timu hiyo, Motshegetsi Mafa na meneja mkuu, Sydney Magagane ambao wote kwa pamoja walitembelea pia makao makuu ya Yanga kwa ajili ya kupata muongozo kwa wenyeji wao.

Makala hii ni kwa hisani ya Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →