Yanga iliondoka mapema leo kuelekea Mali ambako wanakabiliwa na mchezo wa raundi ya tatu kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako
Yanga ilitarajiwa kuwasili Mali jioni na wachezaji kupata mapumziko kabla ya kuanza maandalizi ya kuwakabili Real Bamako katika mchezo ambao utapigwa Jumapili, Februari 26
Hesabu za Yanga katika mchezo huo ni ushindi au kupata alama moja
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi aliondoka na silaha zake zote ambazo zilimpa ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo dhidi ya TP Mazembe
Kiungo Mudathir Yahya ni miongoni mwa wachezaji waliosafiri, akiwa mfungaji wa moja ya mabao ya Yanga katika mchezo dhidi ya TP Mazembe
Nabi alimbadilishia 'Muda' majukumu katika mchezo dhidi ya TP Mazembe akitumiwa katika nafasi ambayo hutumika Stephane Aziz Ki (namba 10)
Huenda kiungo huyo mwenye mapafu ya mbwa akatumika tena katika nafasi hiyo kwenye mchezo dhidi ya Real Bamako
Mwenyewe amesema anafurahia majukumu hayo mapya pamoja na kuwa ni mara yake ya kwanza kutumika kama namba 10
"Nimezoea kukaba kucheza namba sita, nilipopewa nafasi ya juu kuna muda nilikuwa nasahau majukumu nashuka chini lakini wachezaji wenzangu uwanjani wananishtua na kunitaka nirudi juu na ndio maana nakiri kuwa ubora wa timu nzima ndio umenifanya kuonekana bora."
"Nipo tayari kucheza nafasi yoyote kikubwa ni kuipambania timu na kama kocha kaona kitu kwangu akaamua kunipa nafasi siwezi kukataa kufanya kwasababu kazi yangu ni kucheza, naamini baada ya muda nitakuwa bora zaidi," Mudathir alifunguka katika moja ya mahojiano yake baada ya mchezo dhidi ya TP Mazembe
Mudathir sio mchezaji wa kwanza kubadilishiwa majukumu ya profesa Nabi. Ni yeye aliyemtoa Feisal Salum eneo la kiungo namba 6 na kumpeleka namba 10