Yanga ilifunga hesabu za mwezi Februari 2023 kwa mechi ya kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako iliyopigwa nchini Mali na kumalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Mezi March 2023 unaanza kwa mechi ya kwanza siku ya Ijumaa, tarehe 03 kwa mchezo wa kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons ambao unatarajiwa kupigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Katika mwezi huu Yanga itacheza mechi nne mbili zikiwa za kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako na US Monastir zote zikipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Wananchi pia watakuwa na mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Geita Gold ambayo itapigwa March 12

ADVERTISE HERE