Mabingwa wa soka Tanzania , Yanga leo watashuka uwanja wa Azam Complex kuwakabili maafande wa Tanzania Prisons katika mchezo wa kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Mtanange huo wa raundi ya nne, utapigwa saa 1 usiku mshindi atajihakikishia tiketi ya kutinga robo fainali
Kutokana na ukarabati unaendelea kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga imechagua kutumia dimba la Azam kwa mechi zake za nyumbani
Wananchi watautumia uwanja huo hata kwa mechi za ligi kuu zilizobaki kwani dimba la Mkapa litafunguliwa mwishoni mwa mwezi May
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao katika mechi hiyo inayotarajiwa kuwa ngumu
Mara nyingi Prisons sio timu nyepesi hasa inapokuatana na Yanga iwe Dar au Mbeya
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana kwenye ligi katika dimba la Mkapa, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0, likifungwa na Feisal Salum kwenye dakika za lala salama
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi atautumia mchezo huu kama sehemu ya maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako ambao utapigwa Jumatano, March 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa