Mzize anafukuzia ufungaji bora kombe la FA

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Mar 2023
Mzize anafukuzia ufungaji bora kombe la FA

Clement Mzize ndiye kinara wa mabao kwa kikosi cha Yanga katika michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) akiwa amefunga mabao manne

Yuko nyuma kwa tofauti ya bao moja dhidi ya Andrew Simchimba wa Ihefu Fc anayeongoza orodha ya wafungaji kwenye michuano hiyo akiwa na mabao matano

Mzize leo huenda akapewa majukumu ya kuiongoza safu ya ushambuliaji kwenye mchezo raundi ya nne michuano hiyo dhidi ya Tanzania Prisons. Mchezo huo utapigwa uwanja wa Azam Complex, saa 1 usiku

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi huenda akafanya mabadiliko ya kikosi chake kwa kuwapa nafasi nyota wengine ambao hawakutumika katika mchezo uliopita kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako

Ikumbukwe siku ya Jumatano, March 08 Yanga inakabiliwa na mchezo wa pili dhidi ya Real Bamako ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Hii ni mechi ambayo Yanga inahitaji kushinda ili kuweka hai matumaini ya kufuzu robo fainali

Nabi alimpandisha Mzize kwenye kikosi cha kwanza mwanzoni mwa msimu akitokea timu ya vijana. Amepachika mabao saba katika mashindano yote

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’