Mkurugenzi wa Sheria klabu ya Yanga Simon Patrick amemtaka Mwanasheria wa mchezaji Feisal Salum kuacha upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii
Jana kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Fatma Karume ambaye alimuwakilisha Feisal kwenye 'Review case' iliyoamuliwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kusisitiza mteja wake ni mchezaji halali wa klabu ya Yanga, amekuwa akiandika ujumbe mbalimbali akitaka mteja wake aadhibiwe kutokana na makosa aliyofanya kisha aachwe ajiunge na timu aipendayo
Simon amesema ili mkataba uwe umevunjika lazima uthibitishwe na TPLB kupitia Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji lakini Kamati hiyo ilibaini Mkataba ni halali
"Mwambieni Shangazi aache kupotosha watu mitandaoni, Kanuni ya 74(14) TPLB iko wazi, inasema Mkataba wa mchezaji utahesabika kuvunjika pale ambapo taratibu za msingi za uvunjwaji au usitishaji zimefuatwa na kuthibitishwa na Kamati ya Sheria, sasa anavong'ang'ania kulipa fidia kwani uvunjwaji wa mkataba wa kijana umethibitishwa na chombo husika? Sheria ni msumeno," aliandika Simon