Winga Jesus Moloko amewapa sababu mabosi wa Yanga kumuongeza mkataba ili aendelee kuwatumikia Wananchi kwa misimu mingine zaidi
Moloko ni mmoja wa wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu, taarifa za ndani ni kuwa tayari mazungumzo ya kuhuisha mkataba wake yameanza
Kwa sasa ukizungumzia mawinga wa Yanga, basi Moloko yuko katika kiwango bora zaidi kwa kuangalia mchango wake katika timu
Msimu huu amefunga mabao mawili kwenye ligi na kutoa pasi nne za mabao. Pia ana bao moja kwenye michuano ya kombe la Shirikisho akifunga bao hilo katika mchezo dhidi ya Real Bamako
Jana akapigilia msumari wa tatu katika mchezo dhidi ya Geita Gold akiwa amefunga katika mechi mbili mfululizo
Moloko ni winga wa kisasa ambaye mchango wake sio wakati timu inashambulia tu, bali hata wakati timu inapozuia
Yanga inatarajiwa kuboresha eneo la mawinga katika dirisha lijalo la usajili lakini bila shaka panga halitamuhusu Moloko