Kamusoko kurejea kikosi Yanga ikiivaa Township Rollers

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Mar 2018
Kamusoko kurejea kikosi Yanga ikiivaa Township Rollers
Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amethibitisha kuwa kiungo Thabani Kamusoko atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoivaa Township Rollers katika mchezo wa ligi ya mabingwa keshokutwa.

Saleh amesema Kamusoko sasa yuko fiti kwa asilimia 100 baada ya kuwa nje kwa zaidi ya miezi minne.

Kamusoko ni miongoni mwa wachezaji waliokambini kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa March 06 kwenye uwanja wa Taifa kuanzia saa kumi kamili jioni.

Mbali na Kamusoko, kinara wa mabao Obrey Chirwa naye huenda akarejea katika mchezo huo ingawa bado kuna wasiwasi kwa kuwa hakufanya mazoezi siku mbili zilizopita.

Licha ya kuanza mazoezi, mshambuliaji Donald Ngoma hatarajiwi kuwa sehemu ya kikosi kitakachoivaa Township Rollers keshokutwa lakini anaweza kuwa tayari kucheza kwenye mchezo wa marudiano siku 10 baadae kulingana na Meneja wa timu ya Yanga, Bw Saleh.

Beki Vicent Andrew na Amissi Tambwe hawatarajiwi kuwa sehemu ya kikosi pia huku Yohana Nkomola, Juma Mahadhi na Abdallah Shaibu Ò€œNinjaÒ€ nao wakiwa tayari kurejea baada ya kuanza mazoezi na kikosi cha Yanga.

Naye nahodha Nadir Haroub amerejea kikosini baada ya kumaliza msiba wa mwanawe uliotokea wiki mbili zilizopita
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
2h ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
14h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
18h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
23h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’