Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele jana aliitumikia timu ya Taifa ya DR Congo kwa mara ya kwanza katika mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2023 dhidi ya Mauritania
DR Congo waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo huo ulipigwa uwanja wa TP Mazembe, Lubumbashi
Mayele aliingia kwenye dakika ya 87 kuchukua nafasi ya Cedric Bakambu mmoja wa wafungaji wa mabao ya DR Congo
Huo ni mwanzo tu kwa Mayele ambaye katika safu ya ushambuliaji ya DR Congo ni yeye pekee anayecheza ndani ya bara la Afrika
ADVERTISE HERE