Yanga yafafanua uwepo wa Dida kikosini

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
19 Jul 2017
Yanga yafafanua uwepo wa Dida kikosini
Kumekuwa na sintofahamu juu ya uwepo wa mlinda lango Deogratius Munishi 'Dida' ambaye wiki hii ameonekana akifanya mazoezi kwenye kikosi cha Yanga licha ya awali kuripotiwa amekwenda nchini Afrika Kusini kufanya majaribio ya kusakata kabumbu.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema kwa taarifa rasmi aliyonayo, mchezaji huyo amefuzu majaribio yake nchini Afrika Kusini hivyo uongozi umemruhusu afanye mazoezi na kikosi ili kujiweka fiti kabla ya msimu mpya.

Ligi Kuu ya Afrika Kusini inaanza mwezi wa nane sawa na hapa Tanzania.

"Taarifa tuliyonayo, Dida amefuzu majaribio nchini Afrika Kusini. Sisi tumempa nafasi ya kujiweka fiti kabla ya safari yake. Hilo ndiyo jambo pekee lililopo kwa sasa," amesema Mkwasa.

Yanga tayari imesajili magolikipa wawili ambao ni Youthe Rostand na Ramadhani Kabwili anayetarajiwa kutua baada ya mchezo wa Stars dhidi ya Rwanda Jumamosi.

Dida amefuzu majaribio kwenye klabu ya University of Pretoria na atasaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’