Leo ni miaka 51 imepita tangu muasisi wa Taifa la Zanzibar Abeid Amaan Karume atutoke duniani
Karume anatajwa kuwa mchango mkubwa kwa maendeleo ya kisiwa cha Zanzibar lakini pia upande wa Tanzania Bara atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwenye masuala ya michezo
Klabu ya Yanga na hata watani zao Simba wana kumbukumbu ya moja kwa moja ambayo itabaki kwenye historia ya vilabu hivyo kutokana na mchango wa hayati Karume
Hayati Karume ndiye aliyetoa pesa mwaka 1971 kufanikisha ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Yanga lililopo kwenye makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Alifanya hivyo kwa Simba baada ya kushirikiana na wana Simba kupata jengo lao kwenye mtaa wa Msimbazi, Kariakoo,jijini Dar es Salaam mwaka 1971 akichangia kiasi cha pesa katika ujenzi wa jengo hilo pia
Yanga imeendeleza ushirikiano na familia ya Karume na Wazanzibar, historia yake ikiifanya Yanga kuwa klabu pendwa zaidi visiwani Zanzibar
Mke wa Hayati Karume, Mama Fatma Karume ni Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu ya Yanga akidumu kwenye nafasi hiyo kwa miaka mingi