Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dk Dorothy Gwajima ameitangaza Klabu ya Yanga kuwa balozi wa kampeni ya kupinga na kutokomeza mmonyoko wa maadili na ukatili wa jinsia
Dk Gwajima alitangaza Yanga kuwa balozi wa kampeni hiyo katika mkutano na Wanahabari uliofanyika mapema leo katika ukumbi wa Wizara TACAIDS Posta,
"Napenda kuchukua fursa hii kuwatambulisha rasmi Klabu ya Young Africans SC kuwa Mabalozi wa kampeni ya kupinga na kutokomeza mmomonyoko wa maadili na unyanyasaji wa kijinsia na watoto" alisema Gwajima
Akizungumza kwa niaba ya Yanga, Rais wa Yanga, Hersi Said alisema anaungana na Waziri Gwajima katika kampeni hiyo huku akitoa rai kwa klabu za Simba na Azam na nyingine Ligi Kuu kushiriki katika kampeni hiyo
"Napenda kutoa rai kwa klabu za Simba SC, Azam FC, KMC na nyingine zote kuunga mkono kampeni hii, kampeni hii siyo mashindano ya kibiashara sote kwa pamoja tuungane na Waziri kutokomeza changamoto hizi kubwa na kuilinda jamii yetu"
"Wanachama, mashabiki na wapenzi wa klabu zetu ndio waathirika wakubwa wa hii vita dhidi ya ukatili wa kina mama na watoto, tusipowalinda kuna siku tutacheza mpira bila mashabiki uwanjani," alisema Hersi