Simba imeondoka na alama zote tatu katika uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga
Kiwango kibovu kwa Yanga dakika 45 za kipindi cha kwanza ziliwagharimu Wananchi wakiruhusu bao mapema tu dakika ya pili Hennock Inonga akitumia vyema makosa ya safu ya ulinzi katika kucheza mpira wa kona
Bao la pili kwa Simba lilifungwa na Kibu Denis kwenye dakika ya 32 baada ya Yanga kupoteza mpira na kufanyiwa shambulizi la kushitukiza
Kipindi cha pili Yanga ilirejea mchezoni lakini haikuwa rahisi kuipenya ngome ya Simba waliorudi nyuma kujilinda zaidi
Ni mchezo wa pili Yanga inapoteza msimu huu ikiendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi na alama 68 wakati Simba sasa ikisogea ikifikisha alama 63
Sio matokeo mazuri kwa Yanga lakini ndio mpira wa miguu ulivyo muhimu ni kujipanga kuhakikisha mechi nne zilizobaki ushindi unapatikana