Pasipo na shaka katika dirisha lijalo la usajili, Yanga inapaswa kuongeza kiungo mwingine wa ushambuliaji ambaye ataongeza ubunifu katika eneo la mwisho
Kikosi cha Yanga kimesheheni viungo bora sana lakini ni Aziz Ki pekee ambaye ana sifa za kuwa kiungo mtengeneza mabao
kwenye mechi ambazo Aziz Ki ametokea benchi, amebadili taswira ya mchezo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupiga pasi elekezi
Juzi katika mchezo dhidi ya Simba ilikuwa mwendelezo wa umahiri wake hasa anapokuwa katika kiwango bora
Kuingia kwake pamoja na Mudathir Yahya kulirejesha utulivu, alikosa bahati tu kuweza kutumia moja ya nafasi adimu aliyopata katika mchezo huo
Feisal Salum 'Fei Toto' nae alikuwa mzuri sana katika aina yake ya uchezaji lakini hakuwa na sifa za aina ya mchezaji ambaye anarahisisha mambo pale mbele
Yanga inahusishwa kumuwania kiungo wa Singida Big Stars Bruno Gomes ambaye amekuwa na msimu bora kunako klabu hiyo
Kama Rais wa Yanga Injinia Hersi Said atafanikiwa kumuongeza Gomez kwenye kikosi chake basi atakuwa ameleta mtu hasa
Kwa sasa Kocha Mkuu wa Yanga Nasredidne Nabi analazimika kuwatumia Mudathir na Sure Boy katika maeneo ambayo hawawi na ufanisi mkubwa kutokana na changamoto ya 'form' ya Aziz Ki
Sure Boy ni mahiri zaidi kwenye kuifanya timu icheze mpira kutokana na uwezo, umakini wa kupiga pasi fupifupi wakati Mudathiri yeye ni 'box-2-box'
Katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Kagera Sugar na Simba, Aziz Ki ameonyesha kiwango bora na pengine Nabi anaweza kumtumia katika mechi inayofuata dhidi ya Rivers United
Aziz Ki anapokuwa kwenye ubora wake ni mchezaji wa daraja la juu sana ambaye amewahi kushuhudiwa katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara