Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Rivers United unaifanya Yanga iweke rekodi ya aina yake kwa klabu za Tanzania kwenye michuano ya CAF
Yanga imekuwa klabu ya kwanza kushinda mechi tatu ugenini katika msimu mmoja wa mashindano
Walipata ushindi katika mechi dhidi ya Club Africain, TP Mazembe na leo Rivers United
Katika mechi zote ambazo Yanga imeshinda ugenini haikuruhusu bao kutikisa nyavu zake
Mshambuliaji Fiston Mayele yuko kileleni katika mbio za kuwania ufungaji bora Shirikisho akifikisha mabao matano
Kwa hakika huu ni msimu bora sana kwa Wananchi katika michuano ya CAF
ADVERTISE HERE