Tujivunie mafanikio haya, bado hatujamaliza - Arafat

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 May 2023
Tujivunie mafanikio haya, bado hatujamaliza - Arafat

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema kama nchi tunapaswa kumshukuru Mwenye ez Mungu kwa kuweza kufikia mafanikio haya baada ya kuishuhudia Yanga ikitinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika

Arafat amesema ilikuwa shauku kwa nchi kuona timu zetu zinakuwa na nafasi ya kufika katika hatua hizi

"Kila Mtanzania anayeipenda hii nchi yetu Tanzania tunapaswa kumshukuru Mungu kwa hatua ambayo ametufikisha leo kwa Yanga SC kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika"

"Hizi ndizo hatua ambazo kwa Utaifa wetu tulikuwa tunatamani kuziona kwa miaka mingi. Nirudi kwa Wanayanga wenzangu nawapongeza kwa muitikio wenu wa kishindo kwenye mchezo wa leo (jana), mmekuja kwa namba kubwa mkawapa nguvu wachezaji wenu muda wote wa mchezo na hatimae kwa pamoja tukaulinda ushindi wetu wa ugenini vizuri na kutinga hatua hii kubwa kwenye historia ya maisha yetu"

"Wachezaji wetu,makocha wetu Hawa ni mashujaa ambao jasho lao na maarifa yao yataandikwa kwenye kila kitabu cha kumbukumbu isiyofutika kirahisi"

"Viongozi wenu tuliishi na ndoto hizi na Sasa imekuwa, kazi haijaimalizika, kila mmoja wetu aanze kujipanga na mchezo wa Nusu fainali huku tukiendelea na mashindano ya ndani"

"Sio kila mmoja anafurahia mafanikio haya tukasahau kuna makombe yetu mawili ya ndani bado hayajaingia ndani tugeukie kwa kishindo na huko. Nawakumbusha Wananchi Kuna kufuzu kiume na kutolewa kiume sijui sisi tuko wapi na wao wako wapi…..?," aliandika Arafat kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’