Klabu ya Marumo Gallants haijatoa taarifa juu ya ujio wao kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza nusu fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumatano May 10 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Awali kulikuwa na taarifa kuwa wangewasili Alfajiri ya leo lakini haikuwa hivyo pengine watawasili saa sita usiku kwani ndege nyingine kutoka Afrika Kusini itawasili katika muda huo
Jana Malumo Gallants walicheza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mamelodi Sundowns na kuchezea kichapo cha mabao 2-0 katika uwanja wao wa nyumbani
Timu hiyo iko kwenye hatari ya kushuka daraja ikishika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 29, nafasi moja juu ya eneo la kuteremka daraja
Ligi ya Afrika Kusini inashirikisha timu 16 kama ilivyo Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC PL)
Chippa United wanaweza kuwashusha kwenye nafasi ya 15 kama watashinda au kutoka sare mechi yao ya kiporo