Yanga vs USM Alger ni fainali ya kisasi CAF

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 May 2023
Yanga vs USM Alger ni fainali ya kisasi CAF

Wananchi wana dakika 180 za kuwania ubingwa wa kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya ushindi wa jumla wa mabao 4-1 dhidi ya Marumo Gallants katika mchezo wa nusu fainali

Jana Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Marumo katika mchezo wa nusu fainali mkondo wa pili uliopigwa Afrika Kusini huku pia ikishinda mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa wiki iliyopita

Yanga itachuana na USM Alger (USMA) katika hatua ya fainali baada ya Waarabu hao kutoka Algeria kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya ASEC Mimosas katika mchezo wa mkondo wa pili nusu fainali uliopigwa huko Algeria

Timu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa nusu fainali mkondo wa kwanza huko Ivory Coast

Fainali hii itakuwa kisasi kwa Yanga, Wananchi wakiwa na kumbukumbu ya timu hizo kukutana kwenye michuano hii hatua ya makundi mwaka 2018

USMA waliifunga Yanga 4-0 katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi uliopigwa Algeria na Yanga kushinda 2-1 katika mchezo wa marudiano

Wakati huo Yanga ilikuwa ikinolewa na kocha Mwinyi Zahera aliyetua kuchukua nafasi ya George Lwandamina ambaye alirejea kunako klabu yake ya zamani Zesco United

USMA walicheza na ile Yanga inayoitwa ya bakuli kwani ndicho kipindi ambacho Yanga ilikuwa na changamoto kubwa za kiuchumi

Wakati huu itakuwa tofauti! Chini ya uongozi wa Rais Injinia Hersi Said, Yanga imenona na inagawa vipigo kwa kile anayekuja mbele yake

Kikosi cha kocha Nasreddine Nabi kimeiva hasahasa na kina kiu ya kubeba ubingwa wa Shirikisho

Mchezo wa fainali mkondo wa kwanza utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa May 28 na marudiano kupigwa Algeria Juni 03

Yanga inahitaji kutwaa ubingwa hapahapa Tanzania na kwenda kukamilisha ratiba huko Algeria

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’