Baada ya kurejea jijini Dar es salaam kutoka Afrika Kusini mapema leo na kupata saa kadhaa za mapumziko, kikosi cha Yanga kimeondoka Dar kuelekea mkoani Singida wakipitia Dodoma
Jumapili May 21 Yanga itashuka uwanja wa LITI kumenyana na Singida BS katika mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Wananchi wanakwenda Singida wakiwa na lengo moja tu, kushinda mchezo huo ili kutinga fainali
Ni msimu ambao Yanga inawania kushinda mataji manne, mawili (Ngao ya Jamii, Ligi Kuu) yakiwa tayari





ADVERTISE HERE